HEKIMA YA LEO: UNAJUA NINI KUHUSU IMANI? JE, IMANI YAKO NI YA UHAKIKA? SOMA HAPA…

HEKIMA YA LEO: UNAJUA NINI KUHUSU IMANI? JE, IMANI YAKO NI YA UHAKIKA? SOMA HAPA…

1. Imani isiyo na msingi ni imani isiyo na matokeo mema..Wengi huamini vitu vingi, lakini hawajawahi kuuliza msingi wa wanachoamini ni nini?

2. Kuna wanaoamini kitu kwa sababu ni maarufu au kwa sababu kila mtu anaamini hivyo, bado huo si msingi wa imani halisi. Imani halisi haitegemei wingi wa Watu.

3. Ni hatari kujenga imani yako kwa vitu ambavyo havina msingi wowote, ni sawa na kuweka maisha yako mahali pasipo na usalama wala uhakika.

4. Kwa nini unaamini hivyo unavyoamini? Imani yako imekuzalishia nini? Je, chanzo cha imani yako ni nini? Kweli lazima Ijulikane, vinginevyo utapeleka maisha yako pabaya.

5. Kabla hujaamini, tafuta kweli kuhusu hilo jambo. Usidhanie, imani si kitu cha kidhania vinginevyo Itakupa matokeo ya kufikirika tu. Weka imani yako juu ya msingi imara.

6. Msingi imara ni neno la Kristo, maana imeandikwa “Basi imani chanzo chake ni kusikia, kusikia huja kwa neno la Kristo.” Warumi 10:17

IMANI YENYE UHAKIKA!

Sambaza Makala hii...Share on Facebook
Facebook
25Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin
Share on Google+
Google+
0Email this to someone
email

Comments

comments