HIZI NDIZO NAMBA ZA DHARULA ZA KWENYE BIBLIA PALE TUNAPOHITAJI MSAADA

HIZI NDIZO NAMBA ZA DHARULA ZA KWENYE BIBLIA PALE TUNAPOHITAJI MSAADA

Katika maisha ya kawaida ya mwanadamu kuna misukosuko ya hapa na pale ambayo hutokea ghafla pasi kutegemea. Kama ilivyo katika maisha ya kawaida ambapo pindi mtu akumbapo na tukio fulani hupiga namba fulani ili kupata msaada ndivyo ilivyo hata kwenye imani yetu ya ukristo.

Kama ambavyo jeshi la polisi limeweka namba za dharula kwa watu kupiga pindi wakumbwapo na matukio ya wizi ndivyo ambavyo jeshi la mbinguni limetutangazia namba (mistari ya biblia) ambapo tunatakiwa kupiga pale tunapotaka msaada wa jambo fulani.

Twende sambamba

☎📞Katika majonzi, piga Yohana 14
☎📞Watu wakikukosea, piga Zaburi 27
☎📞Kama umetenda dhambi, piga Zaburi 51
☎📞Ukiwa na hofu, piga Mathayo 6:19-34
Katika hatari, piga Zaburi 92
☎📞Ukiona kama Mungu yuko mbali nawe, piga Zaburi 139
☎📞Kama imani yako inahitaji muongozo au marekebisho, piga Wahebrania 11
☎📞Ukiwa mkiwa na mwenye woga, piga Zaburi 23
☎📞Ukiwa mkali (mwenye jazba) na mwenye kupenda kukosoakosoa, piga 1 Wakorinto 13
☎📞Ukijihisi kupata msongo fulani na kuchoka, piga Warumi 8:31-39
☎📞Ukitaka Amani na kupumzika, piga Mathayo 11:25-30
☎📞Iwapo dunia inakusonga na kukufanya umsahau Mungu, piga Zaburi 90
☎📞Ukitaka uhakika wa Ukristu/Kikristu, piga Warumi 8:1-30
☎📞Ukotoka nyumbani kwenda kazini au ukisafiri, piga Zaburi 121
☎📞Sala zako zikiwa kidogo au za kibinafsi, piga Zaburi 67
☎📞Ukihitaji ujasiri kwa ajili ya kazi/jambo fulani, Piga Joshua 1
☎📞Ukifikiri kuhusu kuwekeza/kurejesha, piga Marko 10
☎📞Namna ya kuwa katika mahusiano mazuri na binadamu wenzako, piga Warumi 12
☎📞Kwa ajili ya uvumbuzi/nafasi fulani, piga Isaya 55
☎📞Kwa ajili ya Siri ya Furaha ya Paulo, piga Wakolosai 3:12-17
☎📞Kwa ajili ya fulani, piga Isaya 55
☎📞Kwa ajili ya ufahamu juu ya Ukristu, piga 2Cor 5:15-19
☎📞Umesongwa/umehuzunika, piga Zaburi 27
☎📞Kuwa mwenye kuzaa matunda (mwenye mafanikio/kufanikiwa), piga John 15
☎📞Kama kijitabu chako cha mfukoni kimepungukiwa, piga Zaburi 37
☎📞Kama umepoteza ujasiri mbele ya watu, piga 1 Wakorinto 13
☎📞Kama watu wakionekana hawana ukarimu, piga Yohana 15
☎📞Kama umekatishwa tamaa kuhusu kazi yako, piga Zaburi 126
☎📞Ukiona dunia inakuwa ñdogo na wewe unakuwa mkuu au mkubwa, piga Zaburi 19

🔴Tafadhali tuma hizi namba za dharura kwa watu wote ulio na mawasiliano nao kwa kuwa huwezi jua nani anazihitaji

Sambaza Makala hii...Share on Facebook
Facebook
20Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin
Share on Google+
Google+
0Email this to someone
email

Comments

comments