HIZI NDIZO SABABU ZA KWANINI HUTAKIWI KUIDHARAU NDOTO ULIYOOTA

HIZI NDIZO SABABU ZA KWANINI HUTAKIWI KUIDHARAU NDOTO ULIYOOTA

 

 

Mwalimu Christopher Mwakasege,

Usidharau au usipuuzie ndoto uliyoota
Ni kwa sababu ndoto ni lango la Kiroho ambalo Mungu na Shetani wanalitumia kumfikia mwanadamu. Katika Ulimwengu wa roho kuna ukuta ambao Mungu aliuweka ambao ni mbingu na nchi, na baada ya dhambi kuingia ilitengeneza ukuta kati ya Mungu na mwanadamu. Ndipo Mungu alitengeneza njia za mawasiliano kwa njia ya malango na miongoni mwa malango mengine ni Ndoto. Ukisoma biblia utaona malango mengi sana.

Muda ni lango Mungu yupo kwenye hali ya umilele na aliposema hapo Mwanzo  katika Mwanzo 1:1 ina maana aliukata umilele na alifungua lango la Muda. Yesu ni alfa na Omega yaani Mwanzo na mwisho. Japo yeye hana mwanzo na mwisho . Ili aweze kutusaidia kutembea katika muda, ukiweza kujua namna bora ya kutembea katika muda utakuwa umefaulu sana katika hali ya kimwili na Kiroho.

Ndoto ni lango
Mfano
Mwanzo 41:1-7 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng’ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini.
Na tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng’ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng’ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng’ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.

Farao alipoamka akasema kumbe ni ndoto tu.  Ina maana alikuwa ameidharau lakini bado ilimletea mfadhaiko. Angalia mstari wa nane,  ndoto ya pili aliyoota ya masuke ndiyo iliyomletea mahangaiko sana na kumfanya atafute waganga na wachawi. Lakini hawakuweza kumsaidia, na nisawa na watu wengine ambao wakiota ndoto wanapambana kwenye ndoto na wakijakungundua kumbe ilikuwa ni ndoto wanaona afadhali na hawafuatilii na hata wakifutalia hawajui waombeje kwa sababu hata kujua maana yake inakuwa ni shida.

Farao angeweza kupuuzia na gharama yake ingekuwa ni kubwa sana.  Na Yusufu ndiyo aliweza kutafsiri ndoto yake baada ya waganga na wachawi kushindwa.  Na kupuuzia ndoto ile kungefanya Dunia nzima kwenda vizuri sana kwa miaka 7 na baada ya hapo miaka 7 mingine wangepitia kipindi kigumu sana. Na watu wangejiuliza mbona Mungu hujasema na sisi kumbe aliwaambia.

Mwanzo 41:53-57 Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya Misri, ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri palikuwa na chakula. Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote

Yusufu mume wake Mariam alipewa maelezo kwenye ndoto mara nne na alitii, fikiria angepuuzia ingekuaje…

Mfano wa pili
Ayubu 33:14-19 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake.

Kazi ya ndoto ni kuyafunua masikio yako ya ndani ili waweze kuondoka kwenye makusudia yao yasiyo ya kimungu ndani yao. Na pia kuweza kuwaondoa kwenye mafundisho yasiyo sahihi.

Mfano Kuna mtu mmoja alinisimulia, alipookoka si unajua kunakuwa na mto wa kutafuta chakula na alikuwa anasali hapa na pale, na alikuwa anasali kanisani kwake na akitoka pale alikuwa anaenda na mahali pengine na pengine. Hata katikati ya wiki utakuta anaenda kanisa hili na lile ilia pate mafundisho. Sasa alikutana na kanisa moja akaona limechangamka sana na aliazima kuhamia pale moja kwa moja. Usiku aliota ndoto kuwa Yule mchungaji yupo kwenye njia na watu wanamfuata, mara baada ya muda kidogo akawaona wameingia kwenye majani na mchungaji akiwa mbele , na yeye mwenyewe akawa anawafuata kwa nyuma sasa kabla nae hajaingia kwenye majani akaamka usingizini. Baada ya hapo alijua kuwa ni Mungu anamuambia kuwa asihamie lile kanisa.

Ukiangalia tena Ayubu 33 : 17-19, Mungu anamuondoa mtu kwenye kiburi na kwenye mapenzi yako. Maana kuna watu wanakuwa na kiburi moyoni mwao na wanaanza kuona wao ndio wao na kuna baadhi ya mambo ya kumuuliza Mungu na mengine sio ya kumuuliza Mungu. Kwa sababu hiyo wanakuwa na vikundi vyao na vinakuwa vitovu vya nidhamu na wanakuwa na misimamo yao na kuona hiyo ndio bora sana na hata wanapoteza maana ya wokovu kwa sababu wanakuwa a kiburi sana. Mungu hutumia ndoto ili kuwatoa kwenye mapenzi yao na kuwarudisha kwenye njia nzuri.  Kwa hiyo Mungu anatumia ndoto kufikia nafsi ya mtu na mwili wa mtu.

Kumbukumbu 13:1-4 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

Hesabu 12:6 Kisha akawaambia , sikilizeni basi maneno yangu, akiwapo nabii kati yenu mimi Bwana nitajifunua kwake katika maono nitasema naye katika ndoto.

Aliyeumba lango la ndoto ni Mungu mwenyeshe na shetani anaiga maana yeye hajaumba kitu, bali anatumia malango yaliyoko.  Na malango haya yaliumbwa kwa ajili yetu na biblia inasema tunatakiwa tumiliki malango ya adui. Na sisi kazi yetu ni kuyajua hao malango na kudhibiti shetani asipite hapo.

Mungu anaweza akasema na watumishi wake kwa ndoto, na pia ukitaka kujua ulichoota kwenye ndoto haijalishi kimetokea kiasi gani bali angali matokeo yake maana kama yanakupeleka karibu na Mungu ni sawa ila kama yanakutoa nje ya Mungu basi ujue si ya Mungu hata kama yanatokea kwa ishara kubwa sana na za kutisha, ila kama zinakutoa mbali na Mungu kaa mbali nazo.

Unakuta watu wanajipa vyeo na kuona kuwa ni Mungu kawapa hizo ndoto. Na wakiota ndoto zikitokea katika maisha yao wanasema mimi Bwana nikiota ndoto huwa zinatokea. Na hawaangali mwisho wao,kwa mfano Mungu kakuonesha jambo baya na wewe unaanza kusema kuna hili na litatokea lakini lengo la Mungu kukuonesha doto hiyo ni ili ujue na uweze kuomba ili kupangua hicho kinachotarajiwa kutokea ulichoota.

Watu wengi huwa wanafuata miujiza na ona baada ya miujiza kuomba kwao kunapotea sana, na wanaanza kuwa wazito wa kusoma neno la Bwana. Na hata wakisoma hawaelezi. Muuujiza ni kwa ajili ya Mungu na sio wako ni kwa ajili ni kwa ajili ya Mungu.Wana wa Israel walikula Mana  jangwani na walipovuka kwenda kanani Mungu aliwaambia washike jembe walime.

Mungu aliwaelekeza kwenye maji machungu ili ajifunue kama Yehova Rafa,muujiza umebeba ujumbe, muujiza una sauti ndani,na ndio maana Mungu alikuwa anarudia tena ili waweze kusikia tena.

Ndio maana biblia inasema haijalishi ndoto unayoota ila cheki matokeo yake, au kama umepewa unabii au muujiza isikupe shida ukitokea ila cheki mwisho wake yaani matokeo yake. Ukiona inakupeleka mbali na Mungu wako ujue kuna shida Fulani.

Shetani akija kama shetani inaweza ikawa ni rahisi sana kumjua ila sasa anachofanya anakuja kama malaika wa Nuru  lengo lake ni kukupotosha kwa hiyo kuwa makini sana usiamini kila kitu kama unafuata huo msimamo ulioupata ambao shetani kauleta unakuleta kwenye kiburi na ndio maana na Mungu nae anatumia ndoto ili kukuondoa kwenye hayo makusudi yako yaliyo nje ya mapenzi ya Mungu.

Pia ukipuuzia ndoto ya shetani itakugharimu sana. Kuna watu hawatembei kwenye msimamo wa kanisa la Laiodokia unaosema kumbuka ulipoanguka ukatabu na usipofanya hivyo basi Yesu atakuja kukiondoa kile Kinara chako. Na ujue kuondolewa Kinara ni gharama kubwa sana.

1 Jambo la Kwanza, Jambo unaloota linaweza kujitokeza kwenye nafsi, kwenye mwili wako na nafsi yako.

2 Likiwa na maelekezo na ukayafuata utaona matokeo yake katika maisha yako. Kama ilivyokuwa kwa Farao, Ayubu na katika Kumbukumbu la Torati.

Baada ya kuona ndoto  na nimesoma  ndoto nyingi na wengi hawazilewi na shida kubwa sana niliyoiona ni namba ya kuziombea hizo ndoto.

Na mwingine kwa kutokuwajibika anajipachika cheo kuwa kila nikiota ndoto huwa zinatokea, ila hajui kuwa Mungu anataka upangue hiyo ndoto na badala yake wewe unaanza kutangaza.

 

Sambaza Makala hii...Share on Facebook
Facebook
16Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin
Share on Google+
Google+
0Email this to someone
email

Comments

comments