JE, UMEELEMEWA NA MWOVU? SOMA MISTARI HII SABA KWENYE BIBLIA UPATE KUFARIJIKA

JE, UMEELEMEWA NA MWOVU? SOMA MISTARI HII SABA KWENYE BIBLIA UPATE KUFARIJIKA

Habari yako? Siko yako ama ya rafiki yako inaendaje? Kama basi uko vibaya na unahisi mambo yamekuelemea, ama hata rafiki yako, si vibaya kuigeukia Biblia, maana ni kitabu ambacho kwetu sisi Wakristo, kinaonyesha njia. Mistari yake ina uwezo wa kukubadili na kukufariji pia.
Hivyo basi kama wewe ama rafiki yako amekuwa na siku mbaya, pitia mistari hii na uitafakari ahadi ya Mungu kwako.
1 Petro 5:6-7
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
2 Thesalonike 3:16
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
Wafilipi 4:6-7
Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Zaburi 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza
Mathayo 7:7
Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa
1 Thesalonike 5:16-18
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Comments

comments