NDOTO TUNAZOOTA ZINA MAANA KUBWA KWENYE ULIMWENGU WA KIROHO

NDOTO TUNAZOOTA ZINA MAANA KUBWA KWENYE ULIMWENGU WA KIROHO

Ndugu katika BWANA  YESU shalom. MUNGU akubariki sana popote ulipo na leo nakuletea ujumbe kuhusu ndoto.Kuna watu wanapinga kuhusu uhakika wa ndoto,lakini ukweli ni kwamba Mungu hutumia pia njia ya ndoto kumpelekea mtu ujumbe Mathayo 2;11-15 inayozungumzia Mamajusi pamoja na Yusuphu ambao walipewa ujumbe kupitia ndoto.

Kuna kasumba ya kwamba mtu anaweza kuota kutokana na kile alichokuwa akikiwaza siku nzima ama akikifanya lakini ukweli wa hayo ni kidogo sana kwani ni mstari mmoja tu kwenye biblia ndio unaotofautiana na ndoto Muhubiri 5;3 pia soma mstari wa 7,cha msingi ni kutafakari ndoto uliyoota kama ni mbaya hiyo ni kengele ya hatari unatakiwa uingie kwenye maombi kukemea ili isitimie,

‘Kuna wakati kuna watu wanaota wanakimbizwa na mtu ameshika silaha ama kitu fulani anataka kupigwa nacho,ama wanaota wako katikati ya msitu wanachofanya wanajitingisha ili watoke kwenye hiyo ndoto wakifanikiwa wanahema na kuhema ooh asante YESU nilikuwa naota, hiyo haitoshi ni kwamba umekatisha tu hiyo ndoto kuna siku itakurudia tena dawa yake ni kuomba ulinzi kwa Mungu yawezekana ni kweli kuna mtu anafatilia maisha yako kwa hila”.

Unapoota ndoto kama ya kukimbizwa,au mtu anataka kukuua unatakiwa ujihoji yawezekana ni ishara ya kukuonyesha kwamba utengeneze mambo yako haujakaa sawa, pia tambua  kuwa  MUNGU amezungumza na watumishi wake kupitia ndoto kama 1Wafalme 3;5-10, Ayubu 7;14, Daniel 2;1,Daniel 7;1,.

Aidha  yawezekana unaota ndoto moja zaidi ya mara mbili,yawezekana ya kufanya kitu fulani  ambacho kwa mtazamo na hali uliyonayo unaweza kusema haitaweza kutokea,amesema hiyo ni ishara ya kiroho kwamba hicho kitu kitakuja kutokea cha kufanaya ni kuomba pia kuwa na kawaida ya kuandika kile unachoota  na  na soma pia maandiko  kutoka Hesabu 12;6 pamoja na Ayubu 7;14

Sababu nyingine nyingine ni kwamba asili ya ndoto ni lugha ya roho, ni ujumbe wa Mungu kuhusiana na maisha yako Ayubu 20;8, akasema kama unalala pasipo kuuliza ulinzi wa Mungu na pia kumuomba Mungu akupe ndoto nzuri, shetani atanyemelea nafasi hiyo na kufanya kazi yake,akatolea mfano wa Yusuphu aliyeota wazazi wake na ndugu zake kumsujudia hali ambayo waliipinga sana na ndugu zake kuamua kumuuza kwa wa Misri alipofika kwa Potifa mke wa potifa akataka wafanye dhambi ambayo Yusuphu aliikwepa lakini akajikuta gerezani

Huko nako aliwatafsiri ndoto wafungwa wenzake na ikatokea kama alivyosema kisha kutafsiri ndoto ya Farao iliyokua kumpa uwaziri mkuu kilichotokea ndugu zake walikuja kule kwasababu ya shida ya chakula, yakatimia walimsujudia kama alivyoota, kwahiyo kama una ndoto yoyote maishani omba fanya bidii itimie. na  katika kila ndoto husika na mambo haya kama ni ya mbaya omba maombi yenye nguvu kuzuia katika jina la YESU na kama ni ndoto ya kimungu mshukuru MUNGU kwa maombi na pia kama umeota kibinadamu kwa sababu ya kuliwazia sana jambo hilo basi omba MUNGU ili lile alitakalo yeye ndio litimie. na Ndugu kumbuka kwamba mambo yote huanzia kwanza katika ulimwengu wa roho hivyo hata kama ni ajali hupangwa kwanza katika ulimwengu wa roho ndipo inakuja kutokea hivyo ili mambo mabaya ambayo shetani ameshapanga ili yasije kwetu lazima tuvunje kwa jina la YESU

Mambo hayo wakati mwingine unaweza kuonyesha kwa njia ya ndoto hivyo kemea kwa jina la YESU pia hata mambo mazuri ambayo MUNGU anapanga juu yetu pia wakati mwingine yanaweza kufunuliwa kwetu kwa njia ya ndoto hivyo mshukuru MUNGU kwa maombi.Na mambo haya unaweza ukaota leo na jambo hilohilo likaja likatokea baada ya  yaku mbili mbele au wiki moja,mwezi, mwaka au miaka 3 au zaidi hivyo kudhibiti mapema ni jambo jema sana. MUNGU akubariki sana.
 

Comments

comments